• Breaking News

    NEVER SAY NEVER

    chief kamchicha

    chief kamchicha

    Jumatatu, 11 Mei 2020

    Mkulima Mwamwindi aliyempiga risasi,kumuua Mkuu wa Mkoa Iringa Dr.Kleruu


    Mwanzoni mwa miaka ya 1970 Mkulima said Mwamwindi alikabiliwa na shitaka la kumwua Dr Wilbert Kleruu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa wakati huo.

    Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili . Hivyo, akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke kutoka Nigeria aliukataa utetezi wa Mwamwindi kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu.

    Kuwa ilikuwa 
    siku ya Jumapili , tena siku ya Krismasi, pale Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu, alipofika Isimani na kumkemea Mwamwindi mbele ya wake zake kwa vile alifanya kazi za shamba siku ya Sikukuu.



    Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili . Hivyo, akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke kutoka Nigeria aliukataa utetezi wa Mwamwindi kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu.

    Dr Wilbert Kleruu alikuwa mzaliwa wa mkoa wa Kilimanjaro sehemu iitwayo Mamba (au Mwika), Moshi vijijini ambako siku hizi kunaitwa Vunjo. Alisomea uchumi wa kijamaa hadi ngazi ya PhD, na hasa alikuwa agricultural economist.

    Alifanya kazi kwa karibu sana na Mwl Nyerere ambaye alimpenda sana, maana alimwona ni muumini wa siasa yake ya ujamaa na kujitegemea. Alijituma na kuiamini kwa moyo wake itikadi hiyo, kwamba ukombozi wa nchi utapatikana kwa mapinduzi ya kilimo cha kijamaa (ndio uanamapinduzi anaozungumziwa).

    Alijitahidi pia kutekeleza itikadi hiyo kwa vitendo, na ndiyo iliyomgharimu maisha yake mwaka 1971 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Iringa. Siku moja ya jumapili (hakuwa na jumapili huyu mjamaa) alikwenda kwenye shamba la mkulima mmoja aliyeitwa Saidi Mwamwindi, ambaye alikuwa na shamba kubwa sana, kwa lengo la kufuatilia maagizo yake aliyokuwa ametoa kuhusu shamba hilo, ndipo alipokorofishana na mkulima huyo maana yeye hakuzikubali hata kidogo hizo sera za kijamaa

    Kuwa ilikuwa siku ya Jumapili , tena siku ya Krismasi, pale Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu, alipofika Isimani na kumkemea Mwamwindi mbele ya wake zake kwa vile alifanya kazi za shamba siku ya Sikukuu.

    Inasimuliwa, kuwa Dr. Wilbert Kleruu alifikia hata hatua ya kuanza kudhihaki makaburi ya mababu zake Mwamwindi akimwambia Mwamwindi: "Humu ndimo mlimozika mirija yenu". Alifanya hivyo huku akionyesha makaburi yake kwa kutumia fimbo aliyoshika mkononi. Mwamwindi alikasirika sana. Akaficha hasira yake. Kutoka makaburini, Mwamwindi aliongozana na Kleruu hadi nje ya nyumba yake. Akamwomba Mkuu huyo wa Mkoa abaki nje. Mwamwindi akaingia ndani chumbani.

    Mke wake Mwamwindi alimwona mume wake akichukua bunduki na kusimama dirishani. Mama huyo alidhani mumewe amepanga kwenda kuwinda. Kumbe, Mwamwindi alitokea dirishani na kumwelekea Kleruu aliyedhani Mwamwindi angetoka nje kwa kupitia mlangoni.
    Basi, Mwamwindi akamlenga Mkuu wa Mkoa sawa kichwani. Dr kleruu alinyosha mikono juu na kuomba asemehewe. Mwamwindi alikaa kimya. Kisha akafyatua risasi. Kishindo kilisikika kijijini. Baada ya hapo, kwa mikono yake, Mwamwindi akaubeba mwili wa Mkuu wa Mkoa na kuuweka nyuma ya boneti ya gari alilojia mkuu huyo wa mkoa.

    Mwamwindi alichukua kofia ya pama aliyovaa Kleruu. Akaivaa kichwani na kuanza kuendesha gari hilo hadi kituo cha polisi Iringa. Waliokutana na Mwamwindi njiani walimshangaa akiendesha gari hilo la Mkuu wa Mkoa akiwa amevalia kofia ya mkuu huyo. Hatimaye Mwamwindi akafika kituo cha Polisi.

    Akatoka na kwenda mapokezi. Hapo akaripoti tukio kwa kutamka; " Nendeni mkamchukue mbwa wenu nyuma ya gari!".
    Nyerere alihuzunishwa sana na kifo hicho, na hata kesi ya Saidi Mwamwindi ilipoisha na kupewa hukumu ya kifo, Inasemekana Nyerere hakusita kusaini, na ni mojawapo ya hukumu tatu tu za kifo zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Mwl Nyerere.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Fashion

    Beauty

    Travel