Aliyekuwa kiongozi Mkuu wa Upinzani katika uchaguzi mkuu nchini
Uganda huenda akahukumiwa kifo kama akikutwa na hatia ya mashtaka
yanayomkabili.
Kizza Besigye Kifefe anashtakiwa kwa kosa la uhaini nchini Uganda
baada ya kujiapisha na kujitangaza kuwa yeye ndiyo Rais wa Uganda siku
moja kabla Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni hajaapishwa kushika
wadhifa huo.
Hukumu ya kosa la uhaini (kupindua serikali) ni kifo. Hivyo suala
hili limezua sintofahamu kama kiongozi huyo wa upinzani atahukumiwa kifo
kama akikutwa na hatia.
Wataalamu wa sheria nchini Uganda wanasema kua nafasi ya Kizza
Besigye kushinda kesi hiyo ni ndogo sana kutokana na kile walichosema
kuwa alitangaza hadharani nia yake ya kutaka kuipindua serikali ya
Uganda.
Kizza Besigye ambaye amekuwa akikamatwa mara kwa mara tangu harakati
za uchaguzi kuanza nchini Uganda ameshtakiwa katika mahakama ya Moroto,
Uganda.
Kizza Besigye alijiapisha siku ya Jumatano Mei 11 na kusema ana kila
nyaraka inayothibitisha kuwa yeye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika
mwezi Februari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni