UFUNDISHAJI WA SARUFI
Sarufi ndio kipengele cha msingi katika lugha kwani humpelekea mzungumzaji azungumze na aeleweke kwa ufasaha.
NINI SARUFI?
Ø Ni njia ya
kupanga maneno kwa ufasaha.
Ni njia ambazo kwazo lugha hufikia muundo wake
(sauti, vikundi vya maneno, sentensi,
vikundi vya
sentensi,nk)
Ø Ni utaratibu
wa maumbo na namna maumbo hayo yanavyoashiria maana katika matumizi, mfano;
aina za maneno, mnyambuliko , vihusishi na viunganishi, nk)
Ø Ni kanuni
ambazo zinaweza kuzalisha sentensi za idadi yoyote. Ni sheria zinazotumika
kuunda miundo mbalimbali ya lugha
AINA ZA SARUFI
1.
Sarufi mapokeo (aina za maneno-ngeli
unaangalia umbo lilivyo bila ya kujali litumikavyo katika sentensi)
2.
Sarufi miundo: neno
haliangaliwi lilivyo tu bali na jinsi linavyoleta maana katika sentensi mzima
mf neno moja linaweza kuwa nomino, kivumishi, kitenzi mfano, wale,
mtume
3.
Sarufi zalishi tungo: inaangalia
kwa makini kanuni ambazo zinabadilisha muundo mmoja kuwa mwengine. Mfano
mabadiliko ya wakati katika vitenzi, nk.mfano natumizi ya vitenzi tofauti
(T,Ts,t) yanatupa sentensi sahili, ambatano,utegemezi,
UMUHIMU WA SARUFI
Kuna umuhimu gani kuelewa
au kufundisha sarufi?
Ø Inasaidia
kujifunza lugha nyengine
Ø Inasaidia
katika stadi za kuandika kuzungumza
Ø Inaongeza
ujuzi wa lugha
Ø Kusaidia
kutambua utaratibu wa lugha ulivyo
Ø Kusaidia
kuandika vitabu vya sarufi
Ø Kuweza kutumia
lugha kwa ufasaha
UFUNDISHAJI WA SARUFI
Kwa jumla vipi sarufi
ifundishwe?
Ufundishaji wa sarufi
usitenganishwe na vipengele vyengine vya lugha kama vile kusoma na ufahamu (kwa
mfano unapofundisha kiima na kiarifu fundisha katika ufahamu)
Matumizi ya mifano dhahiri
yasisitizwe (mifano ndiyo itakayoelekeza kupata undani wa kipengele chochote
cha sarufi)
Mfano ufundishapo ngeli
za majina utoe kwanza mifano yake ndio wanafunzi wazitambue aina zake)
Katika ufundishaji wa
sarufi mwalimu afuate kanuni zifuatazo :
Ø Uchaguzi wa aina ya sarufi ambayo itajitosheleza
katika kisw.(mfano sarufi miundo imo katika vidato vyote, sarufi zalishi tungo
kuanzia kidato cha 4-6) (mada)
Ø Sarufi itokane
na utaratibu uliopo katika kisw. Hii itapunguza ufundishaji wa sarufi mapokeo
Ø Uzingatie matumizi
na maana iliyomo katika Kiswahili ili kuepukana na matumizi katika lugha
nyengine. Mfano shangazi langu, ngombe zangu,
Ø Mifano
itokanayo na hali halisi itumike (kutoka kwa wanafunzi wenyewe, vitabuni,
magazetini, nk)
Ø Ufundishaji wa
sarufi uanze na mifano kisha kanuni au sheria zake, kwa mfano kabla ya kueleza
dhana ya kiima na kishazi itolewe mifano ya kiima na kishazi wanafunzi watambue sifa zao
tofauti zao, watoe mifano yao wenyewe ya kiima na kishazi kisha waeleze au
waongozwe kueleza maana ya kiima na kishazi.
Ø Mifano
ilingane na viwango vya wanafunzi na maisha ya kila siku ya wanafunzi sio
maisha ya watu wengine.
Ø Sarufi itokane
na mazoezi mengine ya lugha kama vile kusoma na ufahamu (vifungu vya ufahamu na
makala vitakavyosaidia vitumike , ufundishaji usitoke angani).
Mbunda (1996)
Krashen anasema kuwa grammar
iwe acquired naturally kutoka katika meaningful input na nafasi za kuinteract
katika darasa , isiwe kuna kusomesha miundo na sheria moja kwa moja.
Tricia (2008) anasisitiza mambo yafuatayo Katika
usomeshaji wa sarufi
PPP model:
Presentation: to present new language in context so
that the meaning is clear
To present new form in a
natural spoken or written text so that students can see its uses in discourse
Practice: to help students memorize the form,
to help students produce
word order, to give intensive repetition (Kwa kutumia mifano wagundue sheria za
lugha, new language or grammer).
Production: to reduce control and encourage students to find
out what they can do. Use the form in explaining their own content, see the
usefulness of what they have learned.(watoe mifano yao wenyewe nna waoneshe new
language/rules).
By Hedge Tricia (2008) pg
66
Makala mazuri kwetu walimu ila ningependa kuongeza jambo
JibuFutaTunapofundisha wanafunzi katika sekondari za umma haswa zile za kutwa tunagundua kwamba baadhi ya wanafunzi wanajiunga na shule za upili bila wao kuelewa sheria za kisarufi. Km. Matumizi ya herufi kubwa na ndogo isivyofaa, alama za kuakifisha pamoja hati isiyosomeka. Haya ni baadhi ya mambo yanayochangia mwanafunzi kuhitimu shule kwa misingi "amemaliza" badala ya kuhitimu. Asante
makala nzuri sana, na inatusaidia sisis walimu chipukizi.
JibuFutaBe blessed Sir.