Kwa kifupi Azimio la Tabora ni huisho la Azimio la Arusha, ambao ni msingi mkubwa katika siasa za nchi yetu.
Azimio la Tabora ni msingi wa Itikadi ya Ujamaa wa Kidemokrasia, mrengo wa siasa za Chama cha ACT WAZALENDO.
Kuna utofauti kati ya falsafa ya Ujamaa na kujitegemea, iliyoendeshwa
kuanzia mwaka 1967 chini ya serekali ya Chama cha mapinduzi, kwenye
Uongozi wa Baba wa Taifa na itikadi ya Ujamaa wa Kidemokrasia,
inayofanywa na Chama cha Act Wazalendo.
Kwamba Azimio la Tabora
limechukua baadhi ya misingi ya Azimio la Arusha na si copy and paste ya
Azimio la Arusha, kwa mfano Azimio la Tabora na Ujamaa wa Kidemokrasia
haviongelei na wala havifikirii Kutaifisha Mali halali za matajiri
"nationalization" wawe watanzania au wageni, pili haviongelei wala
kufikiria kupeleka watu vijijini "villagelization".
NINI MISINGI YA UJAMAA WA KIDEMOKRASIA KAMA ILIVYOELEZWA NA AZIMIO LA TABORA.
Sura ya kwanza ya Azimio la Tabora.
Itikadi, falsafa, misingi na madhumuni ya ACT WAZALENDO.
Lengo kuu la uanzishwaji wa chama cha ACT WAZALENDO ni kurudisha jamii
inayozingatia USAWA. Na Lengo hili litafikiwa kupitia mambo yafuatayo.
a) Kuweka sera na mazingira ya kupunguza pengo kati ya walio nacho na wasio nacho (the haves and Have nots)
b) kutoa fursa ya huduma BORA za jamii kwa kila mwananchi zaidi elimu na afya.
c) Kuhakikisha wananchi wanapata fursa kikamilifu kufanya maamuzi kwenye mambo yanayowagusa moja kwa moja.
Katika kupigania jamii yenye Usawa, inayoelezwa kwa ufasaha na Azimio
la Tabora kupitia Ujamaa wa Kidemokrasia, Ngao nne ni tunu kwa ujenzi
huo wa Jamii yenye Usawa.
i) Udugu
Tulifunzwa kuwa binadamu wote ni ndugu na tunaowajibu wa kumsaidia mwenye kuhitaji bila kutegema malipo ya aina yoyote.
Katika siasa za ujamaa wa Kidemokrasia serekali itaweka mfumo wa
HIFADHI YA JAMII utakao toa fursa za elimu iliyo bora, huduma za afya
zenye kukidhi mahitaji na mitaji kwa kujiendeleza kiuchumi bila ubaguzi
wa aina yoyote.
b) Serekali kusimamia Maendeleo ya Nchi.
Serekali kuwajibika moja kwa moja katika uendeshaji wa sekta nyeti,
zenye maslahi mapana ya kiusalama na kiuchumi kwa Nchi bila kuathiri
uwepo wa Sekta Binafsi.
c) Wajibu wa Viongozi na Watumishi wa Umma.
Kuishi na kuenenda katika mienendo inayolinda heshima ya ofisi za umma,
kwa kutokutumia vibaya nafasi zao na kujinufaisha binafsi na ndugu zao
au jamaa zao.
Katika kuhakikisha hili Azimio la Tabora linarudisha MIIKO YA UONGOZI.
c) Demokrasia.
Huu ni msingi wa maendeleo, ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni na
kiuchumi. Demokrasia ni nguzo muhimu ya ujenzi wa taifa linaloheshimu na
kuzingatia utawala wa sheria.
FALSAFA YA ACT WAZALENDO ni SIASA NI MAENDELEO
Karibu katika chama cha wazalendo
ACT WAZALENDO. Taifa kwanza leo, na Kesho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni