Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ameibuka na kuzijibu hoja za Dk. Wilbroad Slaa kuwa yeye ni fisadi aliyeshirikiana na Edward Lowassa katika sakata la Richmond na kwamba alimtishia kumuua.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Rostam amedai kuwa Dk Slaa ni muongo mkubwa na kumtaka Dk Slaa kujitokeza tena na kutoa ushahidi wa kutosha kuwa alimtishia maisha.
“Nilishitushwa na nilisikitika sana, ingawa sikushangaa kusikia tuhuma za Dk Slaa dhidi yangu. Sijawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja naye na madai kuwa nilimtishia maisha yanapaswa kupuuzwa kwa sababu hayana msingi. Kwa nini hakuniripoti polisi badala ya kusubiri miaka yote hiyo kuja kuzungumza hadharani?” Alihoji Rostam Aziz.
Rostam asema kuwa amekuwa na mazoea ya kutoa maneno ya uongo dhidi ya yake na kwamba mwaka 2010 aliwahi kusema kuwa yeye, Edward Lowassa na rais Jakaya Kikwete walikuwa na mkutano Mwanza katika hotel ya Lakairo wakipanga jinsi ya kuhujumu uchaguzi mkuu. Lakini wakati anatoa taarifa hizo, Rostmam anadai yeye alikuwa Afrika Kusini, rais Kikwete alikuwa Lindi na Lowassa alikuwa Arusha.
Katika hatua nyingine, Rostam alikanusha kuhusika na kuifadhili Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Rostam Aziz alitangaza kujiuzulu siasa mwaka 2011 akiliacha wazi jimbo la Igunda na kueleza kuwa amechoshwa na siasa za kuchafuana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni