Nani
alilipia mamilioni ya ukumbi hoteli? Nani aliipia matangazo �live�
katika televisheni? Kwa nini atake makada CCM wamsaidie? Kulikoni
Mwakyembe kuonekana hotelini kabla? Iweje amkomalie Lowassana kutomgusa
Magufuli? Iweje maofisa serikali wamuandalie mkutano wake? Mkutano wake
wagharimu milioni 80.
Siku moja tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa,
kutangaza kujing’atua katika siasa huku akiwashushia tuhuma nzito
viongozi mbalimbali akiwamo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
maswali kadhaa yameibuka juu ya hatua ya kiongozi huyo.Uchunguzi
uliofanywa na Nipashe jana ulibaini kuwa mijadala mbalimbali imeibuka
kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hatua hiyo ya Dk. Slaa, huku
baadhi ya viongozi aliokuwa nao katika kambi ya upinzani wakihoji
maswali kadhaa yasiyo na majibu ya wazi kuhusiana na mkutano wake wa
juzi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkutano wa Dk.
Slaa unakadiriwa kugharimu takribani shilingi milioni 80 kulingana na
takwimu zilivyokusanywa na gazeti hili hapo jana.
Katika mkutano huo
aliozungumza na waandishi wa habari kwa takriban masaa mawili, Slaa
alitumia muda mwingi kumshambulia Lowassa aliyeteuliwa na Chadema
kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha pia vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Mwenyekiti mwenza wa
Ukawa unaoundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na
National League for Democracy(NLD), James Mbatia, ni miongoni mwa watu
kadhaa walioibua maswali yasiyo na majibu ya wazi kuhusiana na mkutano
wa Dk. Slaa.
Akizungumzia Dk. Slaa kumhusisha Lowassa na kashfa ya
Richmond, Mbatia alisema hizo ni njama za kutaka kuwaondoa katika
harakati kampeni za uchaguzi mkuu na kuhoji sababu za katibu huyo wa
zamani wa Chadema kujitokeza juzi na kutoa tuhuma za kashfa hiyo ya
mwaka 2008, huku akiacha baadhi ya kashfa kubwa za ufisadi zilizotikisa
nchi.
Alitaja baadhi ya kashfa ambazo zilitikisa nchi kuwa ni pamoja
na ile ya Tegeta Escrow ambayo kesi dhidi ya wahusika zilipelekwa kwenye
vyombo vya sheria, Meremeta na ile ya wizi wa mabilioni ya shilingi
toka benki kuu kupitia akaunti maalumu ya madeni ya nje (EPA).
Mbatia
alishangaa Dk. Slaa kutozizungumzia kabisa kashfa hizo kama kweli ana
ajenda ya kupambana na ufisadi na kusisitiza kwamba kulikuwa na njama ya
kuwatoa kwenye ajenda ya kampeni za uchaguzi.Hawa wanataka kututoa
kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna haja ya kumjadili,” alisema
MbatiaAkieleza kuhusu kuwania urais kupitia Ukawa, alisema Dk. Slaa
ambaye alipitishwa na Chadema kushindana na wenzake kutoka Cuf (Prof.
Lipumba) na Dk. Kahangwa wa NCCR-Mageuzi, alikuwa akililia urais kwa
kudai kuwa yeye ndiye bora kuliko wenzake na kufanya kikao
kilichomalizika usiku Juni 17 mwaka huu kuvunjika, hivyo siyo sahihi
kudai kwamba hakuwahi kuutaka urais.
Kwa mujibu wa Mbatia, Lowassa
baada ya kujiuzulu akiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama alithibitika
kuwa na kesi ya kujibu, angeweza kushtakiwa kwani Waziri Mkuu anapokuwa
nje ya nafasi hiyo, hana kinga ya kumzuia kushtakiwa.
Alisema Waziri
Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, Ibara ya 33, anatekeleza na kuwajibika kwa majukumu yanayotolewa
na Rais.
Pia alipinga madai ya Dk. Slaa kwamba Lowassa alisema
angekuja na wenyeviti wa mikoa na wa wilaya wa CCM wakati wa kuhamia
Chadema kuwa si ya kweli.
Alisema Dk. Slaa pamoja na wenyeviti wenza
wa Ukawa akiwamo yeye mwenyewe (Mbatia) walishiriki bega kwa bega katika
mchakato wote wa kumleta Lowassa.
Alisema Lowassa hakutoa kauli hiyo
kwamba angekuja na viongozi hao wa CCM, bali alipokuwa bado katika
chama hicho hao walikuwa ni miongoni mwa waliokuwa wanamuunga mkono.
Mbatia
alisema Dk. Slaa alikuwa akililia urais na kusema kuwa yeye ndiye bora
kuliko wenzake na kufanya kikao kilichomalizika usiku Juni 17 mwaka huu
kuvunjika.
Alisema Dk. Slaa ndiye aliyesema asitangazwe kuwa mgombea
kupitia Ukawa Julai 14 mwaka huu mpaka baada ya siku saba ili kulifanya
tukio hilo kuwa la kihistoria.
Mbatia aliwataka wananchi kuepukana na
hoja hizo ambazo ni nyepesi, kwani Ukawa wanasimamia uzalendo, utu,
uadilifu, umoja na uwajibikaji.
Kuhusu wito wa mdahalo kuzungumzia
suala la Richmond, alisema wapo tayari lakini hawawezi kumruhusu mgombea
wao Lowassa kushiriki kwani hiyo ni mbinu ya kuwataka watoke kwenye
reli ya kuendelea na kampeni za uchaguzi mkuu“Hawa wanataka kututoa
kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna haja ya kumjadili,” alisema
Mbatia.Aidha wachangiaji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii nao
waliibua maswali kadhaa kuhusiana na hatua hiyo ya Dk. Slaa.Wakati
maswali kadhaa yakiibuka, jana kulikuwa na taarifa ambazo Nipashe
haikuweza kuzithibitisha moja kwa moja, kuhusu kutokweka kwa Dk. Slaa,
ambaye inadaiwa aliondoka nchini jana.Hata hivyo, Nipashe lilipojaribu
kumtafuta Dk. Slaa kuhusiana na habari za kukimbilia nje, simu yake jana
ilikuwa ikipokelewa na mwanamke ambaye alikana kwamba hiyo siyo namba
ya Mwanasiasa huyo.
MASWALI YALIYOIBULIWA
Baadhi ya maswali
yaliyoibua kizungumkuti kuhusiana na mkutano wa Dk. Slaa juzi ni pamoja
na mlipaji wa gharama za ukumbi wenye hadhi ya juu wa hoteli ya Serena;
mlipaji wa gharama za matangazo ya moja kwa moja kwenye televisheni
tatu; kauli yake ya kutaka asaidiwe na makada wa CCM - Dk. Harrison
Mwakyembe na Samuel Sitta katika kujenga hoja za kudhihirisha kuwa
Lowassa alihusika na Richmond.
Kadhalika, maswali mengine kuhusiana
na mkutano wa juzi wa Slaa ni pamoja na swali kwamba je, bni kwa nini
alimshambulia zaidi mgombea wa Ukawa, Lowassa na kisha kutomgusa hata
kidogo mgombea wa CCM, John Magufuli? Na kwamba je, ni iweje maandalizi
ya mkutano wake yahusishe baadhi ya maafisa wa serikali waliokuwa
wakitumia simu za ofisi ya umma kuwaalika waandishi wa habari?
MBOWE AJIBU KIAINA
"Safari
ya Chadema ni sawa na treni, inayoanzia Dar es Salaam kwenda Kigoma.
Njiani watu wakageuka, na wakaendelea kugeuka katika vituo vingine vya
njiani. Sisi tunaendelea," alisema.
"Chadema siyo mali ya Mbowe wala
kiongozi yeyote. Anayefikiri yeye ni mkubwa hana nafasi... Kamati Kuu
(CC) iliamua, na Mkutano Mkuu uliamua vilevile kuwa Lowassa awe mgombea
wa nafasi ya urais. Kama kuna watu wana mawazo tofauti watatukuta mbele
ya safari," alisema Mbowe wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni
mjini Sumbawanga jana.
CHANZO: NI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni