Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Ndg. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Kamishna Msadizi mwandamizi wa polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Uteuzi wa Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni