Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF na aliyekuwa mgombea wa Urais
kwenye uchaguzi wa Zanzibar, Maalim Seif amepunguziwa ulinzi wa
usindikizi na sasa amebaki na gari moja.
Maalim Seif alikuwa makamu wa kwanza wa Rais katika awamu iliyopita
kabla ya kushiriki uchaguzi wa Zanzibar uliovurugika Oktoba na kususia
uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi Machi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni