Rwanda imetangaza kuwa itajenga njia ya reli ya kisasa aina ya SGR kupitia Tanzania badala ya Kenya ikisema kuwa njia ya Tanzania itahitaji bajeti ya chini ikilinganishwa na Kenya.
Akihutubia waandishi wa habari hapo jana, waziri wa fedha wa Rwanda Claver Gatete, aliongeza kuwa itachukua muda kidogo kujenga reli hiyo kupitia Tanzania badala ya Kenya.
Mwaka 2013 Rwanda, Kenya
na Uganda zilikubaliana kujenga reli itakayoungana na bandari ya Mombasa
kwa gharama ya dola bilioni 13. Reli hiyo ingeigharimu Rwanda dola
bilioni moja za kimarekani. Lakini utafiti uliofanywa na nchi sita
wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki unaonesha kuwa chaguo la
Tanzania litaigharimu Rwanda kati ya dola milioni 700 na 800.
Njia hiyo ya reli itakayotoka Dar es Salaam-Isaka-Kigali/Keza-Musongati (DIKKM) itakamilishwa mwaka wa 2018 na inatarajiwa kugharimu nchi husika jumla ya dola bilioni 5.2.
Njia hiyo ya reli itakayotoka Dar es Salaam-Isaka-Kigali/Keza-Musongati (DIKKM) itakamilishwa mwaka wa 2018 na inatarajiwa kugharimu nchi husika jumla ya dola bilioni 5.2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni