Mwanafunzi wa Kike ambaye ameongoza kitaifa mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2015, Butogwa Shija, amezawadiwa shilingi milioni 5 na benki ya CRDB.
Katika hafla hiyo, Butogwa pia amehakikishiwa ajira ndani ya benki hiyo mara tu atakapomaliza masoma yake.
Bodi ya maendeleo ya Elimu Tanzania, imempatia shilingi laki 5 na kuweka wazi kuwa hii itahamasisha watoto wengi wa Kike kusoma kwa bidii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni