Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema hawezi kugawana madaraka na
kambi ya upinzani kwani alishinda kihalali kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Februari 18.
Akizungumza na kiongozi wa chama cha upinzani cha
Farmers Party of Uganda (FPU), Meja Jenerali Benon Biraaro, Rais
Museveni amesema anakaribisha pendekezo la kufanya mazungumzo na
wapinzani kwa ajili ya kujadili mustakabali wa kisiasa wa taifa.
Alisisitiza kuwa yupo tayari kufanya hilo, lakini akasema hayuko tayari
kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa itakayowashirikisha wanasiasa wa
upinzani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni