ernie Sanders amemshinda Hillary Clinton katika mchujo wa chama cha Democratic uliofanyika katika jimbo la Maine.
Baada ya 91% ya kura kuhesabiwa, seneta huyo wa Vermont ana 64%, huku Clinton akiwa na 36%.
Katika
chama cha Republican, Marco Rubio ameshinda kwa urahisi mchujo katika
eneo la Puerto Rico, na kumbwaga bilionea Donald Trump.
Bi Clinton
na Bw Trump hata hivyo bado wanasalia kuongoza kwa jumla katika
kinyang’anyiro cha kuteua mgombea urais wavyama vya Democratic na
Republican mtawalia.
Jumapili usiku Bi Clinton na Bw Sanders
walikabiliana vikali kuhusu masuala kadha, ikiwemo sera ya kiuchumi,
katika mdahalo wa runingani ulioandaliwa na runinga ya CNN katika mji wa
Flint, Michigan.
Kwenye mchujo uliofanyika Jumamosi, Bw Sanders alishinda majimbo
mawili - Kansas na Nebraska – lakini Bi Clinton akasalia bado kuwa mbele
chama cha Democratic baada ya ushindi mkubwa Louisiana.
Ingawa
ushindi wa Bw Rubio katika eneo la Puerto Rico, linalomilikiwa na
Marekani, utaimarisha matumaini Bw Rubio, ambaye ni gavana wa Florida,
umemzolea wajumbe 23 pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni