Mwanafunzi mmoja raia wa Misri
anakabiliwa na makosa ya kurudishwa nyumbani kutoka Marekani baada ya
kuchapisha katika mtandao wake wa Facebook kwamba yuko tayari kumuua
mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump na
dunia itamshukuru,kulingana na chombo cha habari cha AP.
Emadeldin
Elsayed mwenye umri wa miaka 23,hakabiliwi na mashtaka ya uhalifu
kufuatia ujumbe huo,lakini alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji mwezi
uliopita na atahojiwa ili kubaini iwapo atarudishwa nyumbani Misri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni