• Breaking News

    NEVER SAY NEVER

    chief kamchicha

    chief kamchicha

    Jumamosi, 12 Machi 2016

    OPERESHENI TUMBUA MAJIPU.

    Kwa mujibu wa Rais Magufuli,,,,,, Benki Kuu inawafanyakazi hewa wengi na wanalipwa mishahara na stahiki mbalimbali,,,,,,,, tunapozungumzia kutumbua majipu na kufukuza watumishi wote wasiokuwa waaminifu ni Aibu isiyo kifani kwa kiongozi wa upinzani nchini kupinga Uamuzi wa viongozi wa kitaifa na viongozi waandamizi wanaoamua kuwachukulia hatua kali watumishi wa umma wanaoisababishia serikali hasara za namna hii,,,,,,
    Ni kweli kuwa majipu yote yanayobainika leo yameoteshwa na hata kuiva ktk kipindi chote ambacho CCM ilikuwa madarakani,,,,,,,,,, Lakini hilo haliwazuii viongozi wenye nia njema na nchi hii kurekebisha pale tulipojikwaa,,,,,,,, na ni jambo jema kuwa marekebisho hayo yanafanywa na serikali ya CCM, maana wao (ccm) ndiyo waliochangia matatizo hayo kumea na kunawili
    Sasa ni aibu kubwa, kwa kiongozi wa upinzani mkubwa, kupinga hizo jitihada na kuwatetea watumishi wa umma wasio waaminifu kisa ni mpinzani
    Hii nchi ni yetu sote,,,,,, tusifie zuri kwa pamoja na tupinge baya kwa pamoja bila kujari itikadi zetu

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Fashion

    Beauty

    Travel