Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imetoa taarifa ya kufanikiwa kukamata mtandao wa wezi wa magari yanayoibiwa kutoka Dar es salaam na kwenda mikoani.
Akiongea na vyombo vya Habari jijini Dar es salaam leo Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema jeshi hilo limeendesha Operation mbili ikiwa ni pamoja na kuukamata mtandao huo wa wezi wa Magari na kuwakamata Wanaume na Wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba Jijini Dr Es Salaam.
Kamishna Siro amesema jumla ya magari 24 ya wizi na watuhumiwa 50 wa makosa ya wizi wa magari wamekamatwa ambapo magari hayo yalikuwa yakipelekwa kuuzwa katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Aidha Kamishna Sirro ameitaja operesheni ya kuwakamata wanawake na wanaume wanaouza miili yao pamoja na kununua kuwa imewanasa jumla ya watu 287 katika siku kumi zilizopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni