SAED Kubenea,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers
amekana kumtusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.
Kubenea amekana kumtukana Makonda leo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam wakati akitoa ushahidi wa kesi
inayomkabili kufanya hivyo iliyofunguliwatarehe 15 Desemba mwaka jana.
Kwenye kesi hiyo, Kubenea alifungiliwa madai matatu ambayo ni lugha
ya matusi, kumwita Makonda mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.
Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Thomas Simba ambayo
Kubenea alionekana kuwa na kesi ya kujibu, imeanza kusikilizwa leo baada ya
mbunge huyo kuanza kutoa ushahidi wake.
Kubenea ndiye shahidi namba moja kwenye kesi hiyo ambapo
ameieleza mahakama kwamba, katika vuta nikuvute iliyotokea tarehe 14 Desemba
mwaka jana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es
Salaam hakumtukana Makonda na kwamba, hatua ya kumkatalia kuzungumza na
wananchi si kitendo cha kiungwana.
Kesi hiyo inaendelea kusakilizwa.
Viongozi hao wawili Desemba mwaka jana waligombana kwenye
kiwanda hicho ambapo Kubenea alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri
Makonda .
Tukio lililohusisha kukamatwa kwa Kubenea lilikuwa ni mgomo wa
wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda hicho ambao walimpigia mbunge wao aende
kutatua mgogoro huo ambapo Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na
kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya
kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.
Ilipofika saa 10:30 Makonda alifika na kupata taarifa kwa
muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.
Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika
huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa
Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.
Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia
na kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea)
alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni