Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza
kuiunga mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa
makahaba kuhakikisha biashara hiyo
inakoma nchini.Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema takwimu
zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo
kati ya Watanzania 100 wanaopimwa, sita ni wanawake na wanaume ni wanne
pekee.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Dar es Salaam jana, Ummy alisema si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza
na kuwaacha wateja wao ambao ni wanaume.“Ninalipongeza Jeshi la Polisi
kwa hatua hiyo kwa sababu imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa
kuwakamata wanawake makahaba. Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo
ni wakosaji wanaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tunaungana
na Polisi kushiriki operesheni hiyo,” alisema. Alieleza kuwa, biashara
ya ukahaba inayofanywa na wanawake isingekuwepo endapo wateja
wasingekuwepo, hivyo, wateja wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio
wanaoichochea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni