Haijawahi kutokea. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na uteuzi wa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Dk Carina Wangwe kudumu kwa saa tano tu, kuanzia juzi saa 11.15
jioni hadi saa 4.15 usiku.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Jenista Mhagama ndiye aliyemteua Dk Wangwe na kumtambulisha katika kikao
cha menejimenti ya shirika hilo kilichofanyika juzi na kuhudhuriwa na
watendaji waandamizi wa NSSF, pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo, Antony Mavunde.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, saa tano baadaye Mhagama alitengua
uteuzi huo kwa maelezo kuwa baadhi ya taratibu hazikukamilika. Kutokana
na sintofahamu hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi ombeni Sefue
aliliambia gazeti hili jana kwamba taarifa ya uteuzi wa Dk Wangwe
ilikosewa na kwamba alikuwa ameteuliwa kuwa mwangalizi tu, na siyo kaimu
mkurugenzi mkuu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni