Jaji Mkuu ameyasema hayo leo akiwa katika ukaguzi wa maendelea ya idara ya mahakama visiwani Pemba ambapo pia amezungumzia pia juu ya hali ya kisiasa na uchaguzi wa marudio Zanzibar mapema.
Amesema hadi sasa hakuna pingamizi lolote la kisheria lililoletwa mezani kwa ajili ya kupinga kisheria uchaguzi wa marudio.
Ameongeza pia kuwa wananchi wamegubikwa na ushabiki bila kufuata kanuni na sheria za uchaguzi na kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa sheria huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa amani na utulivu kuhakikisha wanapata viongozi bora.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni