• Breaking News

    NEVER SAY NEVER

    chief kamchicha

    chief kamchicha

    Jumatatu, 7 Machi 2016

    MMOJA WA WAASISI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, AFARIKI DUNIA.


    Mmoja wa waasisi 14 wa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, Hamid Ameir amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
    Alifikwa na umauti jana asubuhi na kuzikwa leo kijijini kwake Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa heshima zote za chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Kifo cha Ameir kimethibitishwa na upande wa ndugu, chama na serikali, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema Ameir atakumbukwa daima kwa mchango wake ambapo baada ya mapinduzi alifanya kazi bega kwa bega na viongozi wenzake kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kutekeleza na kutimiza malengo yaliyoasisiwa katika Ilani ya chama kilichopigania uhuru, Afro Shiraz (ASP)

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Fashion

    Beauty

    Travel