• Breaking News

    NEVER SAY NEVER

    chief kamchicha

    chief kamchicha

    Jumamosi, 5 Machi 2016

    TANGAZO MUHIMU KUTOKA NACTE, KWA UDAHILI WA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.

    BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
    (NACTE)
    TAARIFA KWA UMMA
    KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
    Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi kwa mwaombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya,AstashahadaStashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;
    1. Astashahada na Stashahada
    2. Shahada za Elimu ya Juu
    Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
    1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
    2. Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
    3. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi
    Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
    1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
    2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=
    3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
    4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni Tshs 50,000/=
    Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.
    Imetolewa na: 
    Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi
    4 Machi, 2016

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni

    Fashion

    Beauty

    Travel